- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkoa wa Kagera unaendeleza juhudi za kupanua fursa ya ufugaji nyuki ambapo wafugaji nyuki zaidi ya 200 walipatiwa mafunzo ya ufugaji nyuki kisasa na uongezaji thamani ya mazao hayo. Hamasa na elimu inatolewa kwa wananchi katka ufugaji bora na wa kisasa wa nyuki ili kuongeza uzalishaji wa asali kutoka tani 180 za asali kwa mwaka hadi tani 500 za asali kwa mwaka kwa lengo la kuinua wananchi kiuchumi.
Uzalishaji huu wa asali utatoa fursa ya ujenzi wa viwanda vya kusindika asali, uongezaji thamani asali na mazao yake pamoja na viwanda vya kutengeneza vipodozi na madawa kutokana na matumizi ya asali yakichanganywa na mazao mengine yanayozalishwa Mkoani Kagera mfano karoti na parachichi (avocado).
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa