• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Mamlaka za Serikali za Mitaa
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Maji
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Ajifananisha na Kiwete Aliyeamliwa na Yesu Kutembea Baada ya Kupokea Mguu Bandia na Fedha Taslimu Kutoka Kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera

Imewekwa : January 10th, 2019

“Tangu nizaliwe nikue na nijitambue katika maisha yangu sikuwahi kuona natendewa wema kama siku ya leo na siku ya Jumamosi ya tarehe 29.12.2018, nimekuwa kama yule mlemavu (Kiwete) aliyemuona Yesu na kumuomba amsaidie naye Yesu alimwamuru asimame na kutembea.”

Hayo maneno ni ya Bw. Aron Bukuru Mlemavu mwenyeji wa Kaperanono Kata Nyabusozi Wilayani Biharamulo ambaye ni Mlemavu wa mguu mmoja wa kulia ambapo aliyasema maneno hayo baada ya kupokea mguu bandia na fedha taslimu shilingi  2,023,000/= kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti.

Bw. Aron Bukuru ni Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Kata ya  Nyabusozi Wilayani Biharamulo akiwa katika kikao cha ndani cha chama kilichofanyika Desemba 29, 2018 Wilayani Muleba chini ya Katibu Mkuu Taifa Dk. Bashiru Ally aliomba msaada wa kupatiwa mguu bandia mpya kwani aliokuwa nao ulikuwa umeisha muda wake na ulikuwa ukimuumiza na kumsababishia majereha.

Katibu Mkuu Taifa wa CCM Dk. Bashiru Ally aliendesha harambee katika kikao hicho na Bw. Aron alichangiwa kiasi cha Shilingi 2,723,000/= taslimu ambapo fedha hizo zilikabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti ili kuhakikisha Bw. Aron Bukuru anapata mguu bandia mpya na fedha itakayobaki imsaidie katika matumizi madogo madogo pia na kuweka akiba kwa ajili ya kununulia mguu bandia mwingine endapo huo aliopata ukiisha muda wake.

Baada ya Mkutano ule wa tarehe 29/12/2018 chini ya usimamizi wa Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti Bw. Aron alipelekwa katika Hospitali ya Kagondo Wilayani Muleba na kutengenezewa mguu bandia kwa gharama ya shilingi 600,000/= pia na kupewa shilingi 100,000/= kwa matumizi ya chakula akiwa hospitalini hapo na nauli ya kurudi Nyabusozi Wilayani Biharamulo.

Mara baada ya Mguu bandia kukamilika Januari 10, 2019 Mkuu wa Mkoa Gaguti alifika nyumbani kwa Bw. Aron Bukuku Kaperanono Nyabusozi Wilayani Biharamulo na kumkabidhi kiasi cha shilingi 2,023,000/= fedha iliyobaki baada ya mguu bandia kupatikana. Akikabidhi fedha hizo Mhe. Gaguti alisema kuwa alikuwa natekeleza jukumu aliloachiawa na Katibu Mkuu Taifa wa CCM Dk. Bashiru Ally.

Mwenyekti wa CCM Mkoa wa Kagera Mama Costancia Nyamwiza Buhiye akiongea na ndugu, jamaa na wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais John Pombe Magufuli ni Serikali inayowajali wananchi wake hasa wanyonge wa chini kabisa.

Naye Mama Jonesia Masabile mke wa Bw. Aron Bukuku akitoa shukrani zake kwa Mkuu wa Mkoa alisema kuwa anashukuru mmewe aliyotendewa kwani ilikuwa imefikia mahali mguu bandia aliokuwa nao ulikuwa ukimuumiza na kumchubua jambo ambali lilikuwa likimfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake kikamilifu hasa shughuli za kilimo.

Bw. Aron Bukuku alipata ajali ya gari Ushirombo mwaka 2006 wakati akitokea Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga na kupelekwa Hospitali ambapo ilipelekea mguu wake wa kulia kukatwa na kulazimika kutumia mguu bandia na tangu mwaka 2006 hadi 2018 amekuwa akitumia mguu bandia wa kulia na kila ukiisha muda wake anabadilisha na kununua mguu mwingine ambapo mguu bandia mmoja gharama yake ni kati ya shilingi laki tano hadi  nane.

Matangazo

  • Online Content - inception report for CSA training programme in Kagera region August 19, 2022
  • Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kuhitimishwa Mkoani Kagera Oktoba 14, 2022 August 23, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkoa wa Kagera Wapokea Magari Matano Kusaidi Kufanikisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi

    August 24, 2022
  • Mkuu wa Mkoa Chamila Akagua Miradi na Kuongea na Makarani Wa Sensa ya Watu na Makazi Kagera

    August 23, 2022
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Tazama zote

Video

Kijue Chuo Kipya cha Kisasa cha Ufundi Stadi VETA Mkoani Kagera Kazi Inaendelea.....
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa