- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Maafisa Habari na Tehama Wanolewa Kuziboresha Tovuti za Mikoa na Halmasahuri Ili Kuwa Kitovu Cha Habari Kwa Wananchi
Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na Mradi wa kuboresha Mifumo ya Serikali PS3 waendesha mafunzo ya siku nne juu ya namna bora ya uandishi wa habari za Tovuti za Serikali kwa Maafisa Habari na Maafisa Tehama wa Mikoa na Halmashauri zote Tanzania Bara.
Kutokana na umuhimu wa Tovuti za Serikali hasa katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa nchini kuwa chanzo kikuu cha habari kwa wananchi Serikali kwa kushirikiana na Mradi wa Maboresho ya Mifumo ya Serikali PS3 waliona kuna umuhimu wa kuendesha mafunzo juu ya uandishi bora wa habari katika Tovuti za Mikoa na Halmashauri ili wananchi wapate habari muhimu na zenye uhakika juu ya maendeleo yao.
Kwakuwa siyo Mikoa yote na Halmashauri zote nchini zina Maafisa Habari na kazi za Habari zinafanywa na baadhi ya watu kama Maafisa Tehama, Ofisi ya Rais TAMISEMI na Mradi wa kuboresha Mifumo ya Serikali PS3 wameona kuna umuhimu wa Maafisa hao kupitishwa katika mafunzo ya namna bora ya uandishi wa habari za Tovuti kwa wananchi ili kuwa na uelewa wa pamoja na aina moja ya uandishi (House Style)
Katika Mafunzo hayo mada mbalimbali zihusuzo Uandishi wa Habari zinawasilishwa na wataalamu waliobobea katika mambo ya habari na uandishi wa habari pia ambapo mada hizo ni pamoja na Malengo ya Mwongoz wa Tovuti, Sheria na Maadili ya Habari, Upigaji wa Picha za Kidijitali, Mbinu za Mahojiano, Uandishi wa Aya, Habari katika mfumo wa 5Ws + H (Piramidi iliyogeuka).
Mafunzo ya namna bora ya uandishi wa habari za Tovuti za Serikali yanaendeshwa katika makundi ya mikoa mbalimbali ambapo mikoa ya Geita, Tabora Kigoma na Kagera mafunzo hayo yanafanyika katika Mkoa wa Kagera Bukoba Hotel Manispaa ya Bukoba aidha, mafunzo hayo yalianza Februari 19 na yanatarajia kukamilika Februari 22, 2018.
Matarajio ya Serikali baada ya mafunzo hayo ni kuona Tovuti za Serikali zinakuwa kitovu cha habari kwa wananchi na si ilimradi habari tu bali habari zenye weledi, ukweli, uhakika na kuisemea Serikali inafanya nini katika kuwaletea wananchi maendeleo. Pia katika Tovuti hizo kuwa na taarifa muhimu mbalimbali zinazohusu taasisi husika mfano Mkoa au Halmashauri husika.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa