• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Familia ya Mwanafunzi Aliyefariki Kwa Kupigwa na Mwalimu Yaridhika na Hatua Zilizochukuliwa na Serikali Yakubali Kuendelea na Taratibu za Mazishi

Imewekwa : August 30th, 2018
  • Mkuu wa Mkoa Achukua Hatua kwa Kuagiza Watendaji Wasimamishwe Kazi Kupisha Uchunguzi.

Familia ya Mwanafunzi Marehemu Spelius Erdius (13) aliyefariki baada ya kupigwa na Mwalimu wa nidhamu Respecius Patrick (50) Shule ya Msingi Kibeta Manispaa ya Bukoba yaridhika na hatua zilizochukuliwa na Serikali baada ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti kuwasili kwenye familia ya Mwanafunzi huyo na kutoa ufafanuzi wa hatua zilizochukuliwa na Serikali baada ya tukio hilo kutokea pia na kuwapa pole wafiwa na wananchi wa Kibeta.

Mara baada ya kuwasili katika familia ya Marehemu Spelius Eradius  leo Agosti 30, 2018 majira ya saa 6:00 mchana Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa pole kwa wafiwa na kuongea na familia pia na wananchi wa Mtaa wa Nyamurugo Kata ya Kibeta na kusema kuwa Serikali inaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo pia itahakikisha haki inatendeka kwa kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kushiriki katika tukio hilo.

“Sisi Serikali hatukumtuma Mwalimu Respicius Patrick kufanya aliyoyafanya kwahiyo sheria itachukua mkondo wake na haki itatendeka kwa kila mhusika aliyehusika katika tukio hilo lililosababisha kifo cha Mwanfunzi Spelius Eradis katika Shule ya Msingi Kibeta.” Alisistiza Mkuu wa Mkoa Gaguti.

Aidha, Mhe Gaguti alisema kuwa kutokana na taarifa ya uchunguzi ya kifo cha Spelius Eradius iliyotolewa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kuleta manunguniko kwa familia na baadhi ya wananchi, Serikali iliamua kumleta Mtaalam wa uchunguzi kutoka nje ya mkoa na tayari uchunguzi ulikuwa umefanyika kwa kuwahusisha familia ambayo imekubaliana na uchunguzi huo.

Mara baada ya Mkuu wa Mkoa Gaguti kuongea na familia ya Marehemu Spelius Eradius na wananchi wa Mtaa wa Nyamurugo baba mlezi  wa marehemu Mchungaji Justus Balilemwa alisema kuwa anaishukuru Serikali hasa Mkuu wa Mkoa kuchukua hatua za haraka na kulifuatilia suala hilo kwa karibu ambapo alikubali kuwa sasa familia itaendelea na utaratibu wa mazishi ya Mwanafunzi Spelius Eradius.

Naye Diwani wa Kata ya Kibeta Mchungaji Islael Mlaki kwaniaba ya wananchi wa Kata Kibeta aliushukuru uongozi wa Mkoa ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti katika kulishughulikia suala la kifo cha Mwanafunzi Spelius Eradius  ambalo lilileta taaharuki katika Kata hiyo na alisema kuwa baada ya Mkuu wa Mkoa kutoa ufafanuzi wananchi wameidhika na wataendelea na taratibu za kumuaga mpendwa wao.

Hatua Zilizochukuliwa kwa Watendaji

Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti pia alifika Shuleni Kibeta na kukutana na Walimu, Kamati ya Shule na Wanafunzi ambapo mara baada ya kuongea na kamati ya Shule alisema pamoja na uchunguzi wa Jeshi la Polisi kuendelea lakini pia alimwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba kuunda Kamati ya Uchunguzi ili kuchunguza mwenendo wa utoaji wa adhabu shuleni, Pili kuchunguza kama viongozi waliopewa dhamana ya uongozi kama walikuwa wanawajibika ipasavyo.

Katika Agizo hilo Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti alimwagiza Mkurugenzi wa Manispaaya Bukoba kuwasimamisha kazi Mwalimu Mkuu Bi Renatha Isidory, Mwalimu Mkuu Msaidizi Sunday Elisha na Afisa Elimu Kata Bw. Hashim Mponda ili kupisha uchunguzi wa Kamati iliyoudwa. Kama waliotajwa wakikutwa hawakuwajibika ipasavyo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa na kanuni, taratibu na Sheria za nchi.

Aidha, Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti alimwagiza Mkurugezi wa Manispaa ya Bukoba pia kuisimamisha mara moja Kamati ya Shule hiyo nayo kupisha uchunguzi kama ilikuwa ikiwajibika na kutekeleza majukumu yake ipasavyo katika Shule ya Msingi Kibeta Manispaa ya Bukoba.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwataka wazazi na walezi wa wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Msingi Kibeta kuwaruhusu watoto wao kuendelea kuhudhuria masomo katika shule hiyo kwani hakuna tena tishio katika shule hiyo. Pia wanafunzi wa Darasa la Saba wanatakiwa kujiandaa na Mtihani wa kuhitimu Elimu ya Msingi na hakuna sababu ya wazazi kuwazuia wanafunzi wasihudhurie masomo yao.

Vilevile aliwataka Walimu kuzingatia weledi katika kutekeleza majukumu yao kwa kufauata Sheria, Kanuni na Miongozo ya kazi zao. Na alisema kuwa baadhi ya walimu wamekuwa na tabia zisizoendana na maadili ya ualimu kwani kufuatia tukio hilo pia alipokea malalamiko ya Mwalimu Respicius Patrick mtuhumiwa kuwa kabla ya tukio hilo alikuwa akiwapa adhabu wanafunzi za kuwatoa ngeu na makovu jambo ambao halikubaliki katika utumishi wa umma.

Marehemu Spelius Eradius (13) aliyekuwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kibeta Kata Kibeta Manispaa ya Bukoba anayesadikiwa kufariki dunia Agosti 27, 2018 baada ya Mwalimu wa nidhamu wa shule hiyo  Mwalimu Respicius Patrick kumpiga na kumsbabishia maumivu yaliyopelekea kifo chake mwili wake utaagwa Agosti 31,2018 nyumbani kwa walezi wake Mtaa wa Nyamurugo Kata kibeta na baadae utasafirishwa kuzikwa nyumbani kwa baba yake Mubunda Kijiji Kitoko Wilaya ya Muleba.

                                                                                                                            

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa