• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Bw. Amour Hamad Amour Akiongea Wanafunzi Bugene Sekondari

Imewekwa : August 3rd, 2017

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Awaasa Wanafunzi Kuwa za Nidhamu Ili Kuyafikia Malengo yao Katika Elimu – Bugene Karagwe

Mwenge wa Uhuru  waendelea na mbio zake Mkoani Kagera ambapo tayari umezindua miradi 28 yenye thamani ya shilingi bilioni 8,438,723,915 kwenye Halmashauri za Wilaya tatu Biharamulo, Ngara na Karagwe na miradi hiyo 28 ni kati ya 66 itakayozinduliwa na Mwenge huo katika mkoa mzima ambapo jumla ya thamani ya miradi hiyo ni shilingi bilioni 20,003,692,230.

Mwenge wa Uhuru ukikabidhiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kutoka Wilayani Ngara leo tarehe 3 Agosti, 2017 Mwenge wa Uhuru umezindua miradi 4, umekagua miradi 3 na kuweka mawe ya msingi katika miradi 3 na kukamilisha jumla ya miradi 10 yenye thamani ya shilingi bilioni 2,694,851,845

Aidha, Kiongozi wa Mbio  za Mwenge wa Uhuru Mwaka huu 2017 Amour Hamad Amour  akizindua mabweni mawili ya wavulana katika Shule ya Sekondari Bugene yaliyojengwa kwa gharama ya shilingi 152 milioni fedha za Serikali Kuu,  aliwaasa wanafunzi wa shule ya hiyo yenye kidato cha tano na sita kusoma kwa bidii ili wayafikie malengo yao na malengo ya wazazi wao pia.

Bw. Amour alisema kuwa ili wanafunzi hao waweze kufaulu vizuri ni lazima wawe na nidhamu ya hali ya juu  hasa kwa walimu wao wanaowafundisha pia kujiheshimu wao wenyewe na kuzingatia masomo na maadili wanayofunzwa shuleni hapo.

Pia Bw. Amour aliwapongeza  walimu wa shule hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwafundisha wanafunzi kwa umakini mkubwa na kupelekea kupata matokeo mazuri ya kidato cha sita kwa mwaka 2017. Pia aliwasihi kuhakikisha wanazingatia maadili ya taaluma yao wanapokuwa wanawafundisha wanafunzi hao.

Angalizo, Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2017 alitoa angalizo kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Bugene kuwa ni lazima kuangalia nidhamu za walimu wake na kuchukua hatua mapema kwa  mwalimu atakayekwenda kinyume na maadili ya kazi yake kabla yeye Mkuu wa Shule hajachukuliwa hatua na Serikali ya awamu ya tano.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Mhe. Godfrey Mheruka akimshukuru Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2017 alisema kuwa uongozi wa Wilaya uliamua kupeleka Mwenge wa Uhuru katika Shule ya Sekondari Bugene baada ya shule hiyo kufanya vizuri  katika matokeo yake ya kidato cha sita 2017 ambapo walifaulu kwa ( Daraja la I = 13, Daraja la II =41, Daraja la III =22 na  Daraja   IV =2 aidha hakuna mwanafunzi aliyepata sifuri)

Mwenge wa Uhuru utaendelea na mbio zake Mkoani Kagera  katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa tarehe 4 Agosti, 2017.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa