- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mwenge wa Uhuru Waendelea na Mbio Zake Mkoani Kagera na Kupitia Miradi Yenye Thamani ya Shilingi Bilioni Mbili
Katika siku yake ya pili Mkoani Kagera Mwenge wa Uhuru umeendelea na mbio zake katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba ukikabidhiwa kutoka Wilayani Muleba ambapo katika Manispaa ya Bukoba Mwenge huo uliweza kutembelea, kukagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua jumla ya miradi 13 yenye thamani ya shilingi bilioni 2,185,500,120.
Kati ya miradi hiyo 13 miradi 5 ilizinduliwa, mradi mmoja uliwekewa jiwe la msingi, mradi mmoja ulifunguliwa, miradi mitatu ilikaguliwa, mradi mmoja wa kupambana na dawa za kulevya na miradi miwili ya kugawa vitambulisho vya matibabu kwa wazee. Aidha katika miradi hiyo 13 miradi miwili izinduliwa na mwenge wa uhuru mwaka 2017 na mwaka huu Mwenge ulipita kuona uendelevu wa miradi hiyo
Kati ya midai hiyo 13 ya Manispaa ya bukoba katika upande wa idara ya Afya ulizinduliwa mradi jengo la kutolea huduma za wagonjwa wanaoishi na Virusi vya UKIMWI CTC katika Zahanati ya Buhembe Kata Buhembe, jengo hilo limejengwa na kukamilika pamoja na kuwekewa samani za ndani kwa gharama ya shilingi 83,626,600/=
Mara baada ya kuzindua Jengo hilo Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018 Charles F. Kabeho aliwasisitiza wananchi wanaoishi na Virusi vya UKIMWI kujitokeza kupata huduma ya matibabu mara baada ya jengo hilo kukamilika. Aidha, Kiongozi huyo aliwasisstiza wananchi kutowanyanyapaa watu waishio na Virusi vya UKIMWI kwani unyanyapaa unamsababishia mgonjwa kukata tamaa ya kuishi.
Katika shilingi bilioni 2,185,500,120 ghrama za miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru Katika Manispaa ya Bukoba wananchi walichangia shilingi 762,758,000/=, Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba ilichangia shilingi 24,395,500/=, Serikali Kuu shilingi 331,330,020/= na Washirika wa Maendeleo wa Manispaa ya Bukoba shilingi bilioni 1,067,016,600/=
Miradi 13 iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru katika Manispaa ya Bukoba miradi 11 ni kati ya jumla ya miradi 65 ya maendeleo itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru mkoani Kagera na miradi miwili ni kati ya miradi 15 ya maendeleo ya mwaka jana 2017 itakakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru kuona uendelevu wake kwa kutoa huduma kwa wamnanchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa