• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Mambo Muhimu Kumi Kati ya Mengi Atakayokumbukwa Nayo Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu Akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera

Imewekwa : August 2nd, 2018

Mambo kumi muhimu aliyoyafanya na atakumbukwa nayo kama alama ya utawala wake wa miaka miwili na siku 140 kama Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli Machi 13, 2016 na  kushika kijiti cha kuiongoza Kagera hadi Julai 28, 2018 alipostaafu.

Ulinzi na Usalama: Ikiwa ni ahadi yake mara baada ya kuwasili Mkoani Kagera Mhe. Kijuu wakati akikabidhiwa ofisi na Mtangulizi wake John Mongella Machi 22, 2018 alisema kuwa ujambazi Kagera ungekuwa historia na kweli tangu wakati huo mkoa umekuwa shwali wananchi wakitekeleza shughuli zao za kujenga uchumi bila matukio makubwa ya kutisha ya ujambazi kama hapo awali.

Tetemeko Septemba 10, 2016: Mara baada ya Mkoa wa Kagera kukumbwa na janga la Tetemeko lililotokea Septemba 10, 2016 na kuua watu 17, kujeruhi watu 253, nyumba 840 kuanguka na nyumba 1,264 kupata nyufa Mhe. Kijuu alikuwa mstari wa mbele kuwafariji wananchi wote waliopatwa na janga hilo.

Wakati wa Tetemeko Mhe. Kijuu alisimamia kidete matibabu ya majeruhi ili kupata tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera pamoja na vituo vingine ambavyo vilikuwa vinatoa huduma kwa wahanga wote. Aidha, alihakikisha kuwa taratibu zote za kuwahifadhi wananchi waliopoteza maisha yao zinakamilika kwa kugahrimiwa na Serikali ikiwa ni pamoja na  kutoa rambirambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.

Baada ya Tetemeko Mhe. Kijuu alisimamia ipasavyo Akaunti ya Maafa iliyoanzishwa kwa ajili ya wadau mbalimbali kuchangia maafa ikiwa ni pamoja na kuongoza Kamati ya Maafa Kagera ikiundwa na Mkoa kwakushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha Maafa ambapo jukumu kubwa ilikuwa ni kuratibu michango mbalimali na kuidhinisha matumizi ya michango hiyo na kusimamia urejeshwaji wa hali baada ya Tetemeko kutokea.

Kupitia usimamizi wake mzuri baadhi ya wananchi waliokuwa hawajiwezi kama wazee walipatiwa vifaa vya ujenzi kama saruji, misumari, mabati, nguo chakula na vifaa vinginevyo. Pia Mhe. Kijuu alisimamia vizuri ujenzi mpya wa Shule ya Sekondari Ihungo na Nyakato na Ukarabati wa Shule ya Sekondari Omumwani Manispaa ya Bukoba, Kituo cha Afya Kabyaile Wilayani Missenyi, Ukarabati na Upanuzi wa Kituo cha Afya Kayanga  Wilayani Karagwe.

Aidha, kutokana na uchapaji kazi wa Vikosi vya Jeshi la Wananchi Tanzania Mhe. Kijuu aliomba na kupatiawa kikosi Maalum cha Jeshi la wananchi waliosaidia katika kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa maji kwa wananchi wa maeneo ya vijiji vya Nyakato pamoja na kujenga kituo cha Afya Kabyaile.

Operesheni Ondoa Mifugo Kagera: Tarehe 18 Machi, 2018 Mhe. Kijuu alitoa siku tatu kwa wavamizi wote wa Misitu ya Hifadhi na Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi na Kimisi ambapo mara baada ya siku hizo kuisha iliendeshwa Operesheni kali ya kusafisha mapori hayo na misitu ya hifadhi na kufanikiwa kuondosha zaidi ya mifugo 14,000 ikiwa ni pamoja na kuondosha wahamiaji haramu wote katika Mapori hayo.

Kutokana na mafanikio makubwa ya operesheni hiyo iliyosimamiwa na Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera wanyama wengi waliweza kurejea kwa kasi sana na sasa Serikali imetangaza Mapori hayo kuwa Hifadhi za Taifa. Asante Mhe. Kijuu.

Huduma za Madaktari Bingwa Kagera: Ikiwa ni ahadi yake wakati akikabidhiwa ofisi alipowasili Mkoani Kagera kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali alifanikiwa kusimamia Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kukusanya mapato ya kutosha na kufanikiwa kuleta Madaktari bingwa kwa fedha za ndani za hospitali hiyo baada ya kufunga mifumo ya ukusanyaji wa mapaton. Madaktari hao Bingwa waliweza kutoa huduma za kibingwa kwa wagonjwa 3,146 kati ya 5,700 waliojitokeza kupata huduma.

Katika zoezi hilo lililoendeshwa kwa siku 10 tangu Septemba 18 hadi 28, 2017 Madaktari Bingwa walilipwa kwa fedha za ndani na zilikusanywa kiasi cha shilingi milioni 34,886,3338/=. Aidha, Fedha hizo pia ziligharamia  ununuzi wa madawa na vifaa tiba vilivyotumika katika zoezi.

Kilimo: Mhe. Kijuu akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera aliweza kuhamasisha wananchi kila mara alipopata fursa kuhusu kilimo. Alianzisha kampeini ya kila familia kupanda miche ya miti ya matunda mitano kupambana na utapiamlo. Pia aliwahamasisha vijana kuunda vikundi na yeye kuwasaidia kuwapatia matrekta ya kulima mashamba makubwa ili waweze kunufaika na kilimo.

Magendo ya Kahawa: Kutokana na Serikali kuanzisha mfumo mpya wa ukusanyaji na uuzaji wa kahawa ya wananchi Kagera kupitia Vyama vya Ushirika Mhe. Kijuu alisimamia kidete kuhakikisha hakuna mwanachi yeyote atakayeuza kahawa kimagendo kwa njia ya obutura. Maono yake yalikuwa ni kumuona mkulima akinufaika na kilimo chake bila kuibiwa au kulipwa kiduchu kwa kulaghaiwa na wafanyabiashara.

Elimu: Mhe. Kijuu alisimamia upatikanaji wa madawati katika shule za Sekondari na Msingi, pia alisimamia agizo lake la kuhakikisha kila Halmashauri inakuwa na Shule moja ya kidato cha tano na sita ambapo shule kama Kagemu, Omumwani Manispaa ya Bukoba zilianzishwa, Nyailigamba Muleba, na Murusagamba Ngara zilianzishwa wakati wa utawala wake Mhe. Kijuu.

Afya za Watumishi na Wananchi: Mhe. Kijuu alianzisha utaratibu wa watumishi pamoja na wananchi wote  kufanya mazoezi kila siku ya Jumamosi kila wiki ili uboresha afya zao na kuweka miili yao sawa ili kuepukana na magonjwa nyemelezi. Mkoa wa Kagera ulikuwa mbele kwa kufanya mazoezi kabla ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu kuagiza Watumishi na Wananchi kuwa wanafanya mazoezi mara moja kwa mwezi.

Ushirikianao na Vyombo vya Habari: Mhe. Kijuu alikuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Vyombo mbalimbali Vya habari ikiwa ni pamoja na Waandishi wa Habari bila kujenga matabaka kati yao. Aliwathamini Waandishi pamoja na Vyombo vyao na kazi zao kwa ujumla katika kuhakikisha habari za Mkoa wa Kagera zinasikika ndani na nje ya Mkoa.

Utalii: Mara baada ya kukamilisha operesheni ya kuondoa wavamizi na mifugo katika Misitu ya Hifadhi na Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi na Kimisi na Serikali kutangaza Mapori hayo kuwa Hifadhi za Taifa Mhe. Kijuu alikuwa ameanza kwa kasi sana kuwahamasisha wananchi wa mkoa wa Kagera kuchangamkia fursa za utalii katika maeneo hayo.

Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu umetumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania miaka 40 pia umeongeza miaka miwili na siku 140 za kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Kagera, tunashukuru kwa huduma yako na utumishi uliotukuka. Kagera umetuacha salama tukiwa wamoja kati ya Serikali ya Mkoa na Wananchi wake pia tutaendelea kuyaenzi mazuri yako. Tunasema kwaheri na Karibu tena Kagera ni nyumbani kwako. Tunakutakia mapumziko mema na Mwenyezi Mungu aendelee kukulinda ukiwa na afya njema.

Mwisho: Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu alistaafu katika Jeshi la Wananchi Tanzania Januari 2016 na kuteuliwa  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Machi 13, 2016 na kuapishwa Machi 15, 2018. Alikabidhiwa Ofisi rasmi na Mtangulizi wake Mhe. John Mongella Machi 22, 2016. Aidha, Mhe. Kijuu amestaafu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Julai 28, 2018 na kukamilisha miaka 42 na siku 140 akilitumikia taifa lake la Tanzania kama Mtanzania Mzalendo.

 

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa