• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Mamlaka za Serikali za Mitaa
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Maji
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Mkuu wa Majeshi Tanzania Atembelea Kagera Kukagua Ujenzi wa Kituo cha Afya Kabyaile

Imewekwa : March 3rd, 2017

MKUU WA MAJESHI YA ULINZI TANZANIA AFANYA ZIARA MKOANI KAGERA KUKAGUA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KABYAILE - MISSENYI

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo amefanya ziara ya kikazi Mkoani Kagera kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kabyaile Wilayani Missenyi kinachojengwa upya na Jeshi la Wananchi Tanzania mara baada ya kuathiriwa na Tetemeko la Ardhi lililotokea Mwezi Septemba mwaka jana.

Mkuu wa Majeshi Jenerali Mabeyo alifanya ziara hiyo Machi 2, 2017 na lengo kuu ilikuwa ni kuona maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho mara baada muda alioutoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kuisha mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu 2017.

Rais Magufuli alipofanya ziara Mkoani Kagera Januari 1, 2017 alitembelea eneo la Kabyaile Wilayani Missenyi na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho cha afya na kuagiza kuwa ujenzi huo uwe umekamilika ifikapo Mwisho mwa mwezi Februari 2017.

Mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo Mkuu wa Majeshi Jenerali Mabeyo akiongea na viongozi wa mkoa na wananchi waliofika kumuona kituoni hapo alisema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa katika ujenzi huo, pia alishukuru upanuzi wa majengo kuwa ni manufaa kwa wananchi wa Kabyaile na Wilaya ya Missenyi kwa ujumla.

Pia aliwashukuru wananchi kwa ushirikiano wao na kikosi cha Jeshi la Wananchi Tanzania kinachojenga kituo hicho kuwa kikosi hicho kinafanya kazi katika hali ya utulivu na amani na wananchi wenyeji, aidha aliwaomba wananchi kuwaona wananjeshi kama raia wengine na kuendelea kuwapa ushirikiano  kwani wanatokana na Watanzania wenyewe.

Mkuu wa Majeshi Jenerali Mabeyo baada ya kukagua ujenzi na kupata maelezo ya kina alisema kuwa muda alioutoa Rais Magufuli wa  hadi mwishoni mwa Mwezi Februari 2017 ujenzi haukuweza kukamilika kwasababu kuna kazi zingine za ziada ambazo zilijitokeza na kushindwa kukamilisha kituo hicho kwa muda uliotolewa.

“Kwa kazi alizoelekeza Rais Magufuli tayari zipo katika hatua za mwisho kabisa za umaliziaji, pia na kazi zilizoongezeka zipo katika hatua nzuri ya ujenzi na kufikia mwishoni mwa mwezi Machi 2017 kazi zote zitakuwa zimekamilika zote” Aliwaeleza wananchi Mkuu wa Majeshi Jenerali Mabeyo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Jenerali  Mabeyo alitembelea pia ujenzi wa Shule ya Sekondari Omumwani Katika Manispaa ya Bukoba kunakojengwa vyumba viwili vya mabweni na Kikosi cha Jeshi la Wananchi Tanzania, aidha alimalizia ziara yake katika Shule ya Sekondari Ihungo na kukagua ujenzi mpya wa shule hiyo iliyoharibiwa na tetemeko pia mwezi Septemba Mwaka jana 2016.

Matangazo

  • Online Content - inception report for CSA training programme in Kagera region August 19, 2022
  • Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kuhitimishwa Mkoani Kagera Oktoba 14, 2022 August 23, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkoa wa Kagera Wapokea Magari Matano Kusaidi Kufanikisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi

    August 24, 2022
  • Mkuu wa Mkoa Chamila Akagua Miradi na Kuongea na Makarani Wa Sensa ya Watu na Makazi Kagera

    August 23, 2022
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Tazama zote

Video

Kijue Chuo Kipya cha Kisasa cha Ufundi Stadi VETA Mkoani Kagera Kazi Inaendelea.....
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa