• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Mkuu wa Mkoa Atekeleza Agizo la Rais Magufuli la Kugawa Vitambulisho Kwa Wajasiliamali Wadogo Katika Mkoa wa Kagera

Imewekwa : December 20th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti atekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli la kugawa vitambulisho kwa Wajasiliamli Wadogo ili waweze kufanya shughuli zao za ujasiliamali na kujiingizia kipato chao cha kila siku bila kusumbuliwa na mtu yeyote.

Mkuu wa Mkoa Gaguti ametekeleza agizo hilo la Rais Magufuli Desemba 20, 2018 katika Uwanja wa Uhuru (Maarufu kama Mayunga) Manispaa ya Bukoba ambapo alivigawa vitambulisho hivyo kwa Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Kagera na Halmashauri zake nane.

Kabla ya kugawa vitambulisho hivyo kwa Wakuu wa Wilaya na Baadhi ya wajasiliamali wachache wa Manispaa ya Bukoba Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kuwa Mkoa wa Kagera ulipewa vitambulisho jumla 25,000 vilivyotolewa na Rais Magufuli na kusisitiza  kuwa vitambulisho hivyo vikigawiwa na kuisha uongozi wa mko utaomba vingine zaidi ili kuhakikisha kila Mjasiliamali Mdogo anapata kitambulisho hicho.

Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa angalizo kuwa vitambulisho hivyo vinawalenga Wajailiamali au Wafanyabiashara Wadogo na  wanatakiwa kuwa walinzi wao wenyewe kujilinda ili waweze kujiingizia kipato chao bila kusumbuliwa lakini wasiwe mawakala wa wafanyabiashara wakubwa ili kuwafanyia biashara kwa kutumia vitambulisho hivyo.

“Rais Magufuli alitoa maelekezo kuwa hakuna Mjasiliamali yeyote ambaye atakuwa na kitambulisho na kusumbuliwa, pia na mimi Mkuu wa Mkoa wa Kagera narudia na kuagiza kuwa Mjasiliamali Mdogo yeyote ambaye atakuwa na kitambulisho na kusumbuliwa na mtu yeyote katika mipaka ya Mkoa wa Kagera.” Alisisitiza Mkuu wa Mkoa Gaguti

Aidha, Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwatahadharisha wafanyabiasha wadanganyifu kuwa tayari ofisi yake imepata taarifa kuwa kuna baadhi ya Wafanyabiashara wasio waaminifu kuwa wameanza kupunguza bidhaa kwenye chanja za maduka yao ili waweze kutambuliwa kama Wajasiliamali Wadogo wakilenga kupata vitambulisho. “Ukibainika umefanya mchezo huo hatua kali zitachukuliwa kwa kuzingatia sheria na katika zoezi hili Serikali itasimaia sheria ipasavyo.” Alitahadharisha Mkuu wa Mkoa Gaguti.

Hatua zitakazochukuliwa ni pamoja na wafanyabiashara watakaogundulika kufanya mchezo wa udanganyifu ni pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzani kuwafutia moja kwa moja leseni za biashara. Aidha, Viongozi wa Serikali za Mitaa na Watendaji wa Kata walitakiwa kutenda haki katika utambuzi wa Wajasiliamali Wadogo katika maeneo yao. Pia wananchi walitakiwa kupaza sauti pale watakapoona zoezi hilo linaendeshwa bila kutenda haki.

Naye Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kagera Bw. Adam Ntoga alitoa ufafanuzi wa ni Mjasiliamali yupi Mdogo anatakiwa kupata kitambulisho ambapo alisema kuwa ni Wajasiliamali wadogo ambao hawajawahi kutambuliwa na mfumo wa kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na mzunguko wao wa fedha haufikii kiasi cha shilingi milioni nne. Pia Bw. Ntoga alisema kuwa malipo ya kitambulisho hicho ni shilingi 20,000/- tu.

Katika Mkoa wa Kagera Wilaya ya Bukoba ilipatiwa jumla ya vitambulisho 3,580 na Wilaya za Missenyi, Karagwe, Kyerwa, Ngara, Biharamulo na Muleba kila Wilaya kupitia Wakuu wa Wilaya zilipatiwa vitambulisho 3,570 na kukamilisha jumla ya Vitambulisho 25,000 vilivyotolewa katika Mkoa wa Kagera na Rais Magufuli Desemba 10, 2018

Ikumbukwe kuwa Desmba 10, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli  akiwa Ikulu Jijini Dar es Salaam alitoa vitambulisho vya wajasiliamali wadogo 670,000 kwa Wakuu wa Mikoa yote na kila Mkoa ulipatiwa vitambulisho 25,000 na Mkoa wa Kagera ukiwemo ambapo Rais Magufuli alisema kuwa kila Mkuu wa Mkoa atakusanya shilingi 500 milioni kupitia vitambulisho hivyo.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa