- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti atoa mkono wa heri ya Eid El-Fitr na kuwatakia heri na baraka Waislamu wote Mkoani Kagera pamoja na Tanzania katika sikukuu hizo na kuwataka washerekee kwa amani na utulivu.
Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa mkono huo wa heri Juni 4, 2019 katika msikiti wa Bilele Manispaa ya Bukoba alipokutana na viongozi pamoja na wajumbe wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) mkoa wa Kagera lililoongozwa na Sheikhe wa mkoa wa Kagera Kharuna Kichwabuta na kuwapongeza kuelekea kumaliza mfungo mtukufu wa ramadhani na kuanza Sikukuu za Eid El-Fitr.
“Nimeona nije kuwapongeza mnapoelekea kumaliza Mfungo Mtukufu wa Ramadhani na kuelekea katika Sikukuu za Eid El-Fitr ili niwatakie heri na sikukuu njema kama ilivyo destuli yetu katika mkoa wa Kagera sisi Serikali kushirikiana na madhehebu ya dini katika shughuli mbalimbali kwa hiyo tunawatakia heri pia na sherehe njema za Eid El-Fitr.” Alifafanua Mkuu wa Mkoa Gaguti.
Aidha, Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwahakikishia Waislamu wote mkoani Kagera kuwa sikukuu za Eid El-Fitr zitaadhimishwa kwa amani na utulivu kwani Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Wilaya zimejipanga kuhakikisha sikukuu hizo ziaadhimishwa kwa amani na upendo kama ilivyo desturi ya wananchi wa Kagera.
Vilevile Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa angalizo kwa wazazi na walezi wa watoto kuchukua tahadhari katika Sikukuu za Eid El-Fitr kutowaruhusu watoto waende katika maeneo ya fukwe wakiwa wao wenyewe bila kuwa chini ya uangalizi wa walezi wao ili kuepukana na matatizo yanayoweza kujitokeza baadae ikiwa ni pamoja na watoto kuzama ziwani au kupotea.
Akipokea mkono wa heri ya Eid El-Fitr kwaniaba ya Waislamu wenzake Sheikh Kharuna Kichwabuta alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Kagera na Serikali ya mkoa kwa ujumla kuwatakia heri Waislamu wote katika sikukuu zao za Eid El-Fitr wanapoelekea kumaliza Mfungo Mtukufu wa Ramadhani. Pia Sheikh Kichwabuta aliomba na kusisitiza umoja na mshikamano kati ya Waislamu na Serikali uendelee kama ilivyo mila na desturi ya mkoa wa Kagera.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa