- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Aridhishwa na Ufanisi wa Mradi wa Kusaidia Waathirika wa Tetemeko Mkoani Kagera
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) nchini Tanzania Bw.Fred Kafeero afanya ziara ya siku tatu Mkoani Kagera kuona shughuli za mradi wa kusaidia kaya 5000 katika Halmashauri za Bukoba, Bukoba Manispaa, Kyerwa Missenyi na Muleba zilizoathiriwa na Tetemeko la Ardhi Septemba 10, 2016.
Baada ya Tetemeko la Ardhi Septemba 10, 2016 Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) lilitoa msaada wa mbegu za mazao mbalimbali yanayovumilia ukame kama mihogo, viazi lishe, mahindi ya muda mfupi na migomba inayovumilia magonjwa, mbuzi wa maziwa, ufuaji wa kuku na ufugaji wa samaki ili kuzikomboa familia hizo 5000 na baa la njaa na kuinua kipato kwa ngazi ya familia.
Bw. Kafeero akiwa mkoni hapa na kutembelea baadhi ya kaya zinazonufaika na mradi FAO alisema kuwa ameridhishwa na ufanisi wa mradi huo katika kaya hizo ambapo mafanikio yanajionesha yenyewe kwa wanakaya hao kunufaika na mbegu ambapo mashamba yapo, ufugaji wa kuku na samaki unaendelea vizuri.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu akiambatana na Bw.Fred Kafeero katika ziara hiyo alimhakikishia Mwakilishi Mkazi huyo kuwa mkoa unafanya ufuatiliaji wa karibu sana kwa kaya 5000 zilizonufaika na mradi ili kuhakikisha zinakuza kipato kupitia mradi kwa kupata chakula pamoja na ziada ya kuuza na kupata kipato cha fedha.
Aidha, Mhe. Kijuu aliendelea kuwasisitiza wananchi wanaonufaika na mradi wa FAO kuhakikisha wanafanyakazi kwa kujituma ili mradi unapomalizika mwaka 2019 wawe wameweza kujikomboa katika shida za chakula pamoja na kipato pia kuiendeleza miradi yao wenyewe bila kutegemea Shirika la Umoja wa Mataifa.
Kwa ujumla Mradi FAO umeongeza uzalishaji wa chakula, umeongeza kipato kwa wananchi na kupunguza umasikini, umeboresha lishe kupitia maharage ya lishe (yenye madini ya chuma na zinki na protini) na viazi lishe vyenye vitamin A. Pia radi umeongeza uzalishaji na upatikanaji wa mbegu bora wa mazao yanayovumilia ukame na magonjwa.
Aidha, mradi umekua kiunganishi kati ya watafiti na wakulima kwenye teknolojia ya kilimo (Research Extension Farmer Linkage) kwa njia ya mafunzo kupitia Mashamba darasa (Farmer Field Schools FFS). Mradi tayari umetoa msaada wa mafunzo kwa kaya 2500 kuanzia Julai 2017 hadi sasa. Pia Bw. Kafeero baada ya kufurahishwa na kilimo kizuri cha mihogo aliwahaidi wakulima katika kijiji cha Nsambya kuwanunulia mashine ya kuchakata mihogo.
Aidha, gharama za mradi hadi Februari 2019 utakapokuwa umekamilika ni takribani Shilingi Milioni 700 Ziara ya Bw. Kafeero Mkoani Kagera ni ya siku tatu kuanzia tarehe 23 hadi 25 Januari, 2018.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa