• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Atoa Taarifa ya Serikali Juu ya Kifo Cha Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kibeta Manispaa ya Bukoba

Imewekwa : August 29th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawiro kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera ametoa taarifa ya Serikali juu ya kifo cha Mwanafunzi Spelius Eladius (13) wa Shule ya Msingi Kibeta Manispaa ya Bukoba anayesadikiwa kufariki dunia baada ya kupigwa na Mwalimu Respecius Mutazangira ambaye ni Mwalimu wa nidhamu wa shule hiyo ya Kibeta kwa kutuhumiwa kuiba pochi ya Mwalimu Elieth Gerald.

Mkuu wa Wilaya Deodatus Kinawiro akitoa taarifa ya Serikali kwa Vyombo vya Habari leo Agosti 29, 2018 alisema kuwa mara baada ya tukio hilo kutokea siku ya Jumatatu Agosti 27, 2018 Serikali ilichukua hatua mara moja kwa kuwakamata watuhumiwa wanaotuhumiwa kufanya kitendo hicho ambao ni Mwalimu Respecius Mutazangira (anayetuhumiwa kumpiga mtoto na kumuua), Mwalimu Elieth Gerald (aliyetoa taarifa kuwa amebiwa pochi yake) pamoja na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo.

Baada ya kuwakamata watuhumiwa hao Jeshi la Polisi Mkoani Kagera linaendelea kufanya uchunguzi ikiwa ni pamoja na kuwahoji Walimu waliokuwepo wakati tukio hilo linatokea  ili kukamilisha uchunguzi wa tukioa na mara baada ya kukamilisha uchunguzi watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani.

Mkuu wa Wilaya Kinawiro alitoa rai kwa wananchi hasa wazazi wa watoto wanaosoma katika shule hiyo ya Msingi Kibeta kuacha kuwazuia wanafunzi kwenda shuleni hapo kuendelea na masomo yao kwani hali tayari imetulia na Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi lakini pia Serikali inaendelea kuifanyia kazi taarifa ya uchunguzi ya Kidaktari iliyotolewa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa juu ya sababu zilizosababisha kifo cha Mwanafunzi Spelius Eladius.

“Jana asubuhi siku ya Jumanne tarehe 28 Agosti, 2018 nilifika Shule ya Msingi Kibeta na kukutana na Walimu na Wanafunzi niliongea nao na kuwahakikishia kuwa Serikali inaendlea kufanya kazi kuna kuwataka walimu kuendelea  kufundisha na watoto waendelee kuingia madarasani. Lakini pia leo tarehe 29 Agosti, 2019 nimeenda shuleni hapo kuangalia hali lakini nimekuta kuna baadhi ya wazazi wamewazuia watoto wao kwenda shuleni, natoa wito kwa wazazi wawache watoto waende shule kwani hakuna tishio lolote shuleni hapo.” Alitoa wito Mkuu wa Wilaya Kinawiro.

Aidha, Mhe. Kinawiro alitoa wito kwa wananchi wa Bukoba kutulia na kuiamini Serikali yao kwani tukio hilo linaendelea kufanyiwa kazi na taarifa zitakuwa zinatolewa mara kwa mara na Serikali hasa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili wananchi wajue kila kinachoendelea katika kuhakikisha haki inatendeka na wananchi wanapata taarifa sahihi jinsi kifo cha mwanafunzi huyo kilivyotokea na ni nini kilisababisha kifo hicho.

Pia Mhe. Kinawiro alito wito kwa Walimu katika shule Mkaoni Kagera kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kulingana na kanuni, taratibu na sheria na kuzingatia kanuni na miongozo ya utoaji wa adhabu kwa wanafunzi watakaobainika kuwa na makosa lakini wasichukue hatua za kutoa adhabu holela bila kufauta kanuni za utoaji wa adhabu hizo na kusababisha madhara kwa wanafunzi.

Mwanafunzi Spelius Eladius (13) wa Shule ya Msingi Kibeta Manispaa ya Bukoba anasadikiwa kufariki dunia Agosti 27, 2018 muda mfupi baada ya kupigwa viboko na Mwalimu Respecius Mutazangira Mwalimu wa shue ya Msingi Kibeta na kusabisha kifo chake baada ya mwanafunzi huyo kusadikiwa kuwa ameiba pochi ya Mwalimu Elieth Gerald asubuhi alipompokea Mwalimu huyo mizigo yake lakini baadae ilikuja kugundulika kuwa hakuwa ameiba pochi hiyo. Uchunguzi wa suala hili unaendelea na taarifa zitatolewa na Serikali kadri suala hili linavyofanyiwa kazi.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa