• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

RC- Gaguti Azindua Rasmi Msimu wa Ukusanyaji wa Kahawa Kagera 2019 Bei ya Malipo Awali Yatangazwa Vyama Vikuu Vya Ushirika Kuanza Kulipa Julai Mosi 2019

Imewekwa : June 29th, 2019

Msimu wa ukusanyaji wa kahawa mwaka 2019/20 kutoka  kwa wakulima hadi Vyama vya Msingi wazinduliwa  rasmi  Mkoani Kagera ikiwa ni pamoja na malipo ya kwanza kutangazwa kwa vya Vikuu vya Ushirika vya KCU 1990 Limited na KDCU Limited kuwa yatakuwa ni shilingi 1,100 kwa kila kilo moja ya maganda.

Akizindua rasmi msimu huo wa ukusanyaji wa kahawa Juni 29, 2019 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gagiuti Wilayani Kyerwa Nkwenda aliwahakikishia wakulima kuwa msimu huu wa 2019/2020 Serikali imejipanga kuondoa changamoto zote zilizojitokeza msimu uliopita na mkulima atanufaika na kahawa yake na kulipwa kwa wakati.

Mkuu wa Mkoa  Gaguti akiongea na wakulima wa Kahawa na wananchi waliokusanyika kumsikiliza  Nkwenda Kyerw alisema kuwa tayari Vyama Vikuu vya Ushirika Mkoani Kagera tayari vimepewa Shilingi Bilioni saba na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania aidha,  wakulima ambao tayari wamekusanya kahawa yao kwenye Vyama vya Msingi wataaanza kulipwa malipo ya awali ya shilingi 1,100/= kwa kila kilo kuanzia Julai 1, 2019.

Mhe. pia Gaguti alisema kuwa Serikali imejipanga vizuri msimu huu wa 2019/2020 kuhakikisha wakulima wanalipa fedha zao kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuhakikisha fedha hizo hazipiti katika mikono mingi ya viongozi wa Vyama vya Msingi bali kila mkulima atalipwa fedha zake kupitia akaunti yake ya benki ili kudhibiti upotevu wa fedha zilizokuwa zianapotea au kutumika bila idhini ya wakulima wenyewe.

Naye Mtendaji Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Japhet Justine akiongea na wakulima Wilayani Kyerwa Nkwenda alisema kuwa Benki ya TADB  mwaka jana 2018 ilitoa zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa wakulima 148,000 na mwaka huu watahakikisha wanatoa fedha kwa wakati na imfikie mkulima moja kwa moja kupitia mfumo wa benki.

“Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua akaunti jumuishi za wakulima ili wakulima wasikatwe fedha zao hata kama ni senti moja ilipwe moja kwa moja kwa mkulima na sisi TADB tutahakikisha tunalipa fedha hizo kupitia akaunti za benki.”Alisistiza Mtendaji Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania Bw. Japhet.

Katika kuondoa changamoto za msimu uliopita wa mwaka 2018 Mkuu wa Mkoa Gaguti akikagua Chama cha Msingi Rwabwere na kujionea namna ya kupima kahawa za wakulima alisema kuwa lazima kilo zote na pointi ziandikwe na mkulima ahakikishe. Pia fedha za mazidio za wakulima zisitolewe maamuzi na viongozi wa Vyama vya Msingi bali wakulima wenyewe ndiyo waamue zifanye nini.

Aidha, mkuu wa Mkoa Gaguti na ujumbe wake walikagua shamba bora la mkulima Bw. Abdu Ndegeza na kuona kahawa bora na zilizokomaa zikivunwa. Tayari Chama Kikuu cha Ushirika cha KDCU Limited tayari kimekusanya kilo milioni 3,200,000 matarajio yake ni kukusanya kilo milioni 35,000,000. Msimu wa Mwaka jana 2018 Vyama Vikuu vya Ushirika Mkoani Kagera vilikusanya jumla  kilo milioni 58.9  na msimu huu vyama hivo vinatarajia kukusanya zaidi kilo milioni 52.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa