- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti atembelea kiwanda cha Kagera Sukari kilichoko Wilayani Missenyi na kuhaidi kushughulikia masuala makuu matatu ambayo yanasababisha kiwanda hicho kuzalisha sukari ya kutosha lakini kwasasa inakosa soko kutokana na sukari kutoka nje ya nchi kuingizwa kimagendo katika masoko ndani ya nchi.
Akiwa kiwandani hapo Septemba 18, 2018 lengo likiwa ni kutembelea kiwanda hicho na kuona changamoto ambazo zinasababisha sukari kukwama kwenda sokoni Mkuu wa Mkoa Gaguti baada ya kupokea taarifa ya kiwanda hicho iliyowasilishwa kwake na Meneja Mkuu wa Kiwanda Bw. Ashwin Rana alibainisha mambo makuu matatu ambayo alisema kuwa atayafanyia kazi ili kutatua changamoto ya sukari ya magendo kutoka nje ya nchi.
Kwanza, Magendo ya Sukari kutoka nje ya nchi, Mkuu wa Mkoa Gaguti akilitolea ufafanuzi suala hilo alisema kuwa hayupo tayari kuona suala hilo linaendelea katika Mkoa wa Kagera na atahakikisha anakomesha magendo ya sukari kwa njia yoyote ile ili kulinda soko la kiwanda cha Sukari Kagera. “Kwa kutumia Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na wananchi tutahakikisha suala hilo linakomeshwa mara moja.” Alifafanua Mkuu wa Mkoa Gaguti.
Pili, Mkuu wa Mkoa Gaguti ili kutatua kero ya sukari kutoka Kiwanda cha Sukari Kagera kukosa soko na kupelekea kiwanda hicho kuwa na shehena kubwa ya sukari ambayo haitoki alitoa ushauri kwa uongozi na menejimenti ya kiwanda hicho kuangalia upya mfumo wao wa usambazaji wa sukari katika masoko kuwa rafiki kwa wafanyabiashara na usiokuwa na mashariti magumu sana ili kuhakikisha sukari inasambaa kila kona kudhibiti sukari ya magendo kutoka nje ya nchi katika soko la ndani.
Tatu, Mkuu wa Mkoa Gaguti aliushauri pia Uongozi na Menejimenti ya kiwanda cha Kagera kuangalia bei ya sukari yao katika masoko ili kuendana na bei ya viwanda vingine vya nchini kiushindani jambo ambalo litapunguza ushindani wa wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu kuingiza sukari ya magendo kutoka nje ya nchi au kuagiza sukari kutoka katika viwanda vya mikoa mingine wakati Kagera kunzalishwa sukari ya kutosha.
“Hivi karibuni natarajia kukutana na Wakuu wa Mkioa ya Kanda ya Ziwa Mkoani Shinyanga katika mambo muhimu nitakayozungumza nao mojawapo ni suala la kudhibiti magendo ya sukari na kuona namna bora ya kuhakikisha kiwanda cha Sukari Kagera kinasambaza sukari katika mikoa hiyo na kuweka mikakati endelevu ya kuvilinda viwanda vyetu vya ndani maana nimejionea shehena ya suakari ilivyo hapa ni ya kutosha.” Alisisitiza Mkuu wa Mkoa Gaguti
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa Gaguti alipongeza juhudi za kiwanda hicho katika uwekezaji kwa kuweza kuzalisha hadi tani 75,000 za sukari kwa msimu wa mwaka 2017/2018 ulioishia mwezi Juni 2018. Pia alipongeza juhudi za kiwanda kuzalisha ajira 6,000 kwa wananchi wenye takribani familia 30,000. Aidha, alipongeza huduma zinazotolewa pia kiwandani hapo kwa jamii mfano huduma za matibabu zinazotolewa bure kusaidia wafanyakazi na wananchi wanaozunguka kiwanda cha Sukari Kagera.
Kiwanda cha Sukari Kagera tangu kuanza uzalishaji wa sukari katika msimu wa mwaka huu 2018/2019 mwezi Julai tayari kimezalisha jumla ya tani 26,000 za sukari na matarajio ya uzalishaji kwa msimu mzima ni tani 84,000 za sukari. Aidha, tani 12,800 za sukari bado hazijaingia sokoni na bado zipo katika kiwanda hicho kutokana na tatizo la sukari ya magendo katika masoko.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa