- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kambi ya Umishumita Mkoani Kagera Yaaswa Kuchagua Vipaji Halali na Si Mamluki Ili Kuleta Ushindani Kitaifa – CP Athumani
Katibu Tawala Mkoa wa Kagera CP Diwani Athuman ambaye ni Mwekiti wa Michezo Mkoani Kagera afunga rasmi mashindano ya UMISHUMITA ya mkoa kwa kutoa rai kwa wakufunzi na Walimu wa michezo kuhakikisha wanafuata vigezo vilivyotolewa na Serikali kuunda timu bora isiyokuwa na mamluki itakayoshiriki mashindano hayo ngazi ya Kitaifa na kuleta ushindi.
Katibu Tawala CP Athumani alitoa rai hiyo chuoni Katoke Wilayani Muleba kwenye kambi ya mashindano ya Mkoa yaliyohusisha shule za Msingi kutoka Halmashauri za Wilaya za Mkoa wa Kagera ambapo mara baada ya kushindanishwa katika michezo mbalimbali inatakiwa kuundwa timu moja kila mchezo itakyowakilisha Mkoa katika Mashindano ya Kitaifa Jijini Mwanza.
Rai hiyo ilitolewa na Katibu Tawala wa Mkoa Juni 10, 2018 baada ya Afisa Michezo Mkoa Bw. Kepha Elias kueleza kuwa katika kambi hiyo wanakumbana na changamoto kubwa ya baadhi ya Halmashauri za wilaya kutaka kwenda tofauti na maelekezo ya Serikali ya kuzingatia umri wa watoto wanatakiwa kushiriki mashindano hayo lakini pia kuwahusisha Mamluki Wasiokuwa walimu kuendesha mashindano ya michezo hiyo
“Ndugu mgeni Rasmi kuna baadhi ya Halmashauri za Wilaya zinaleta watoto wasio na vigezo vya kushiriki mashindano ambapo umri ni miaka 14 lakini shule kwa kushirikiana na walimu wanawaleta watoto waliozidi umri huo, pia wanashirikisha walimu mamluki yaani walimu wasiostahili kufundisha michezo na kuwahalalisha kushiriki katika zoezi hili tofauti na maelekezo ya Serikali.” Alisisitiza Bw. Kepaha
Katibu Tawala CP Athumani alisisitiza sana kuwa mkoa haupo tayari kufanya kinyume na maelekezo ya Serikali bali Maelekezo na miongozo itazingatiwa kwa kufauata vigezo vilivyopo na kama ikitokea maelekezo hayo yamekiukwa atakikisha anamchukulia hatua yeyote atakaekuwa amehusika kwa njia moja au nyingine.
MAAGIZO
Mwekiti huyo wa Michezo Mkoani Kagera CP Diwani Athumani alitumia fursa hizo kuziagiza Halmashauri za Wilaya kwanza kuahakikisha Maandalizi ya Michezo ya UMISHUMITA katika ngazi za Wilaya yafanyike mapema sana ili kuhakikisha katika Ngazi ya mkoa wanaletwa watoto wanamichezo wenye vipaji haswa.
Pili ni kuhusu michango ya fedha kwa ngazi ya Mkoa, Kila Halmashauri ya Wilaya ihakikishe inatoa michango yake mapema ili maandalizi kwa ngazi ya mkoa ifanyike mapema kuliko ilivyokuwa mwaka huu kwani fedha hizo zinatolewa na Serikali kwahiyo hamna sababu ya ucheleweshwaji kutoka katika Halmashauri za Wilaya.
Tatu Kila Halmshauri ya Wilaya kuhakikisha kila wiki ya pili ya mwezi inashiriki kikamilifu katika michezo ambapo wananchi wote na watumishi wanatakiwa kushiriki katika mazoezi ili kuweka miili yao sawa na kujikinga na magonjwa yanayosababishwa na kutoafanya mazoezi , aidha watoto nao washirikishwe kwani wakijengewa utamaduni huo wa kufanya mazoezi wakiwa wadogo watauzoe na kuwa sehemu ya maisha yao.
Mwisho Mkuu wa chuo cha Ualimu Katoke akiishukuru Serikali ya Mkoa kufanyia kambi ya Michezo kwa Watoto wa Sekondari na Shule za Msingi chuoni hapo alisema michezo hiyo imewapa changamoto ya kurekebisha mitaala yao na masomo ya michezo kuyapa umuhimi ili walimu wanaohitimu katika chuo hicho waweze kwenda kuwafundisha watoto michezo shuleni.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa