• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Mamlaka za Serikali za Mitaa
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Maji
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Waziri Suilemani Jofo Akizindua Madarasa Matano Yaliyokarabatiwa Katika Shule ya Msingi Ihembe Wilayani Karagwe

Imewekwa : May 11th, 2018

Waziri Jafo Azindua Miradi Mitatu ya Maendeleo na Kuleta Neema ya Hospitali Tatu za Wilaya Mkoani Kagera

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleimani Jaffo aweka mawe ya msingi katika miradi miwili ya afya na kuzindua mradi mmoja wa elimu Mkoani Kagera ambapo miradi hiyo imetolewa fedha na Serikali kwa ajili ya kuboreshwa na kutoa huduma stahiki kwa wananchi.

Waziri Jafo mara baada ya kuwasili mkoani kagera Mei 11, 2018 alianza ziara yake Wilayani Karagwe ambapo alizindua miradi miwili, mradi wa ukarabati wa vyumba vya madarasa vitano ujenzi wa vyoo matundu manane na ujenzi wa chumba cha stoo katika Shule ya Msingi Ihembe shule iliyojenwa mwaka 1948 na ilikuwa haijawahi kufanyiwa ukarabati hadi mwaka 2017.

Waziri Jafo alizindua shule hiyo baada ya Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kutoa fedha jumla ya shilingi milioni 66 kufanya ukarabati katika shule hiyo ambayo ilikuwa na hali mbaya sana. Waziri Jafo aliridhia kutoa fedha hizo baada ya utembelea shule hiyo mwaka 2017 na kuona ubovu wa miundombinu ya shule hiyo.

Aidh, katika hatua nyingine Waziri Jafo aliweka mawe ya msingi katika Kituo cha Afya cha Kayanga Wilayani Karagwe na Zahanati ya Maruku Wilayani Bukoba. Katika kituo cha Afya Kayanga Serikali ilitoa shilingi milioni 670.7  ikiwa milioni 170.7 zilitolewa na mfuko wa Maafa Mkoa wa Kagera baada ya Tetemeko la Ardhi kutokea Mkoani Kagera Septemba 10, 2016.

Fedha hizo milioni 170.7 zilikuwa za kujenga  wodi ya wazazi, chumba cha kuhifadhia maiti, na nyumba ya kuzalishia umeme. Vilevile Serikali ilitoa milioni 500 kwaajili ya kujenga Jengo la wagonjwa wa nje, Nyumba ya mganga , chumba cha upasuaji, wodi ya wanaume, jengo la utawala na njia za kutembelea ambapo kazi hizo zote zimekamilika kwa asilimia 95.

Akiongea na wananchi Waziri Jafo katika miradi hiyo aliyoweka mawe ya msingi na kuzindua alisema kuwa Mkoa wa Kagera una bahati ya kupata fedha za miradi ambapo katika mwaka wa fedha 2018/2019 Ofisi ya Rais TAMISEMI imetenga fedha bilioni 105 za kujenga hospitali za Wilaya nchi nzima na mkoa wa Kagera umepata bahati ya Hospitali tatu katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Wilaya ya Karagwe na Kyerwa.

“Tangu uhuru nchi nzima ilikuwa na hospitali za Wilaya 77 tu hadi mwaka 2018 lakini sasa Serikali imetenga bilioni shilingi 105 kwa ajili ya kujenga Hospitali za Wilaya 67  nchi nzima na Kagera imepata hospitali tatu kama nilivyo taja hapo awali, haya ni mapinduzi makubwa katika Sekta ya Afya yatakayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano,” Alifafanua Waziri Jafo.

Pia Waziri Jafo alisema kuwa tanga uhuru hadi mwaka 2018 nchi ilikuwa na Vituo vya Afya 115 lakini sasa Serikali imeamua kujenga vituo vya afya na kufikia idadi ya 208 na vituo hivyo vimejengwa kisasa kwa kuzingatia kuwa huduma zote lazima zipatikane katika vituo hivyo hasa huduma za upasuaji wa akiana mama wajawazito.

Waziri Jafo aliwaagiza  Wakurugenzi wote wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa kuhakikisha wanatoa mikopo kwa vikundi vya akina mama na vijana bila riba kwani fedha hizo zinazotolewa zinakuwa zimekusanywa kutoka katika kodi za wananchi wenyewe.

Ziara ya Waziri Jafo itaendelea Mei 12, 2018 Katika Manispaa ya Bukoba na Halmashauri ya Bukoba Pamoja na Kamati ya Bunge katika Shule za Sekondari Nyakato na Ihungo zinazojengwa upya baada ya kuharibiwa na Tetemeko la Ardhi Septemba 10, 2016.  

Matangazo

  • Online Content - inception report for CSA training programme in Kagera region August 19, 2022
  • Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kuhitimishwa Mkoani Kagera Oktoba 14, 2022 August 23, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkoa wa Kagera Wapokea Magari Matano Kusaidi Kufanikisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi

    August 24, 2022
  • Mkuu wa Mkoa Chamila Akagua Miradi na Kuongea na Makarani Wa Sensa ya Watu na Makazi Kagera

    August 23, 2022
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Tazama zote

Video

Kijue Chuo Kipya cha Kisasa cha Ufundi Stadi VETA Mkoani Kagera Kazi Inaendelea.....
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa