Mkoa wa Kagera
Na.
|
AINA YA TAARIFA
|
MAELEZO
|
|||
1.
|
JINA KAMILI NA UTAMBULISHO
|
Profesa Faustin Kamuzora
|
|||
2.
|
TAREHE YA KUZALIWA
|
|
|||
3.
|
Elimu au Mafunzo
|
Jina la Shule/Chuo
|
Kutoka Mwaka |
Hadi Mwaka |
Kiwango (Mfano Cheti/Shahada)
|
i |
Doctor of Philosophy (PhD), Informatics |
Chuo Kikuu cha Bradford
|
2003 |
2006 |
Shahada ya Uzamivu Katika Teknolojia ya Habari
|
ii |
Masters of Science, Agricultural Economics |
Chuo Kikuu cha Jimbo la Carolina Kaskazini cha Kilimo na Ufundi
|
1994 |
1996 |
Shahada ya Uzamiri wa Sayansi na Kilimo cha Biashara ya Kimataifa.
|
iii |
Bachelor's degree, BSc Agriculture (Rural Economy) |
Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo
|
1985 |
1987 |
Shahada ya Sayansi ya Kilimo Vijijini
|
iv |
Elimu ya Sekondari Kidato cha V & Vi
|
Shule ya Sekondari Old Moshi
|
1981 |
1983 |
Cheti Elimu ya Sekondari
|
v |
Elimu ya Sekondari Kidato cha IV
|
Seminari ya Katoke
|
1977 |
1980 |
Cheti Elimu ya Sekondari
|
vi |
Elimu ya Msingi
|
Shule ya Msingi Rwambaizi
|
1970 |
1976 |
Cheti Elimu ya Msingi
|
4. |
Uzoefu na Ajira
|
Kampuni/ Taasisi |
Nafasi |
Kutoka Mwaka |
Hadi Mwaka |
i. |
Katibu Tawala wa Mkoa
|
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
|
Katibu Tawala |
2019 |
- |
ii. |
Katibu Mkuu (Sera na Uratibu)
|
Ofisi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
|
Katibu Mkuu |
2017 |
2019 |
iii. |
Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Muungano na Mazingira)
|
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
|
Katibu Mkuu |
2016 |
2017 |
iv. |
Katibu Mkuu (Mawasiliano) Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
|
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
|
Katibu Mkuu |
2016 |
2016 |
v. |
Mtafiti, Mkufunzi, Mwezeshaji, Mshauri na Mtawala Chuo Kikuu cha Mzumbe.
|
Chuo Kikuu cha Mzumbe
|
Mtafiti, Mkufunzi, Mwezeshaji, Mshauri na Mtawala
|
1992 |
2015 |
vi. |
Mchumi wa Kilimo na Afisa Kilimo wa Wilaya
|
Wizara ya Kilimo
|
Afisa Kilimo Wilaya |
1988 |
1992 |
|
Karani wa Benki
|
National Bank of Commerce (NBC)
|
Karani |
1984 |
1984 |
Faustin Kamuzora ni Profesa, Mwandishi wa vitabu mbalimbali, Mchambuzi, Mshauri, Mtawala na mwana rotari anayependa kujifunza, mwenye shauku juu ya uongozi wa huduma za jamii, pia ni mbobezi na mzoefu kwa miaka 30 katika Taaluma ya Utawala wa Umma. Amechapisha majarida kadhaa ndani na nje ya nchi aidha, ameandika vitabu vinne juu ya mbinu mbalimbali za utafiti wa maendeleo ya kiuchumi, amekuwa mkufunzi na mkaguzi mkuu wa kitaaluma kwa Taasisi kadhaa za Elimu ya juu, ndani na nje ya nchi.
Faustin Kamuzora amewahi kuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Utawala na Fedha) - Chuo Kikuu Mzumbe kwa miaka nane pia akiwa mkufunzi mbobezi, mwezeshaji na mshauri. Ameongoza na kushiriki katika warsha mbalimbali za mafunzo katika nyanja za maendeleo na uongozi, mifumo fikira, usimamizi wa mifumo ya Habari, maendeleo ya kiuchumi na usimamizi wa kimkakati.
Profesa Faustin Kamuzora kwa sasa ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera ambapo kabla ya hapo alikuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu. Profesa Kamuzora pia amekuwa Katibu Mkuu (Mawasiliano) Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na baada ya hapo alikuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira. Aidha, amekuwa mwakilishi wa Afrika Mashariki katika Bodi Kuu ya Jukwaa la Kilimo na Ushirika Vijijini katika Bara la Afrika, Caribbean, Pacific na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (ACP / EU).
Akiwa mwana rotari, alikuwa Rais wa Morogoro Central Club na Gavana Msaidizi wa Rotari ya Morogoro na Dodoma, mjumbe wa timu ya Rotari 9211, 2014-2015. Kamuzora ni Mume na Baba wa familia anayependa kusoma vitabu malimbali na anapendelea kusafiri sehemu mbalimbali duniani. Huyu ndiye Profesa Faustin Kamuzora Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa